FEDERER APONEA KIPIGO AUSTRALIAN OPEN
Nyota wa tenisi Roger Federer, 38, ameponea kipigo toka kwa M-australia John Millman mchezaji amabaye hayupo kwenye viwango vya ubora. Ni katika mechi iliyochezwa kwa saa 4 na dakika 3 ikivutia mashabiki zaidi ya 15,000 waligawana washabikia wachezaji hawa katika uwanja wa Rod Laver Arena.
Akiwa nyuma kwa 8 – 4 katika ‘tie-break’ ya kuamua matokeo, alishinda pointi 6 mfululizo na kuweza fanikiwa pata ushindi wa seti 4-6 7-6 (7-2) 6-4 4-6 7-6 (10-8).