NGASSA NA KABWILI WAFUNGIWA, KOCHA WAO AKIPEWA ONYO KALI
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB) Steven Mguto ametangaza kufungiwa mechi tatu na faini ya Tsh laki tatu kwa wachezaji wa Yanga, Ramadhani Kabwili, Mrisho Ngassa, Cleofas Sospeter na Mbeya City Kelvin John na Majaliwa Shaban, waliokuwa wanategeana kutoka uwanjani hadi Polisi walipolazimika kuingia uwanjani na kuwatoa.
Kitendo ambacho kinatafsirika kama kugoma kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo, tukio hilo lilitokea wakati wa timu hizo zilipo maliza kufanya mazoezi ya kupasha misuli moto kabla ya mchezo kuanza
Hata hivyo pia bodi ya Ligi kupitia kamati ya saa 72 imempa onyo kali kocha wa Yanga Luc Eymael na kuagiza Yanga itoe tamko kufuatia kocha huyo kumtuhumu muamuzi Hance Mabena kuwa alimbagua kwenye mchezo Azam FC ikishinda 1-0 dhidi ya Yanga.