MZEE KUKAA NYUMBANI KUNABOA – GUARDIOLA
Akiwa anasherekea kutimiza umri wa miaka 49 siku ya leo, Kocha Pep Guardiola atakuwa uwanjani dhidi ya Roy Hudgoson mwenye miaka 72 ikiwa ni tofauti ya miaka 23 kati yao. Guardiola alikuwa na umri wa miaka 5 kipindi Hudgoson anachukua kibarua chake cha kwanza nchini Sweeden katika klabu ya Halmstad.
Akiulizwa maoni yake kuhusu kufundisha hadi umri wa Hudgoson, Guardiola alisema “Ukiwa katika mazoezi katika umri wa miaka 72, nadhani kukaa nyumbani patakuwa panaboa. Kazi yetu ni nzuri sababu unafanya kazi na Vijana wadogo walioko katika mashindano. Kila mchezo ni tofauti labda ndio maana Roy na makocha wengine wa umri mkubwa bado hawajastaafu. Sisemi nitastaafu wiki ijayo ila sidhani kama nitakuwa nikifundisha katika umri huo.”
Tokea awe kocha amefanikiwa shinda idadi nzuri ya mataji ikimfanya kuwa moja ya makocha wenye mafanikio katika soka. Ametwaa:
UEFA – 2
Super Cup – 3
Club World Cup – 3
EPL – 2
LaLiga – 3
Copa deL Rey – 2
Supacopa de Espana – 3
Bundesliga – 3
DFB Pokal – 2
FA Cup – 1
Community Shield – 2