CONOR MCGREGOR KUREJEA ULINGONI UFC WIKIENDI HII
Baada ya kuwa nje ya mchozo wa MMA kwa miezi 15, Conor McGregor atarejea ulingoni weekend hii kpigana na Donald ‘Cowboy’ Carrone jijini Las Vegas nchini Marekani.
Conor alitangaza kustaafu mchozo huu wa MMA baada ya pambano lake na Khabib Nurmagomedov kuisha kwa kupigwa Oktoba 2018.
Pamoja na pambano hili kutokuwa la ubingwa Conor amesema anategeme kuingiza pauni millioni 80 pitia pambano hili.
kwa miezi 15 aliyokuwepo nje ya ulingo Conor amekuwa akikitangaza kinywaji chake cha pombe kali kiitwacho ‘Proper Twelve’ mbacho amejinasibu kuwa kimemuingizia dola billioni 1 ndani ya mwaka wake wa kwanza sokoni.
Conor bado anabakia kuwa mchezaji muhimu katika utangazaji na uuzaji wa mchezo huu wa MMA akiwa amefanikiwa uza (sold out) mapambano yake 6 kwa nyakati tofauti huku pambano lake na Nurmagomedov likiwa linashikilia rekodi ya kulipiwa na watu zaidi ya milioni 2.4 kutazama katika mtandao.
Conor anatarajia pata upinzani toka kwa Cerrone mwenye rekodi nzuri y akushinda mapambano 23 na mwenye kuujua vizuri mchezo huu.