YANGA YAKIRI KUTOLIPA MISHARA MIEZI MIWILI NA KUWA NA DENI LA ZAIDI YA TSH BILIONI 1
Klabu ya Yanga SC chini ya mwenyekiti wake Dkt Mshindo Msolla leo imeongea na waandishi wa habari na kubainisha mambo mbalimbali kuhusiana na klabu hiyo, hususani habari zinazoendelea mitandaoni kwa sasa kuwa wachezaji hawajalipwa.
Yanga kupitia Dkt Msolla imekiri kuwa haijalipa wachezaji wake kwa miezi miwili ila kufikia leo jioni watakuwa wamekamilisha changamoto hiyo, Dkt Msolla pia amekiri kuwa kinachoigharimu klabu yao ni pamoja na madeni waliyoyakuta ambayo ni zaidi ya Tsh bilioni 1.2.
“Tumekuwa na madeni ya aina kama nne moja ni deni la serikali kwa maana ya kodi kwa TRA ambalo linafikia kama Tsh milioni 800, deni jingine kubwa tulilolikuta ni ada za usajili ambazo wanadai wachezaji ni Tsh milioni 254, kama hiyo haitoshi tulikuwa na madai ya makocha waliokuwepo na wasiokuwepo”
“Mfano yule Hans van Pluijm tumekuta deni la Tsh milioni mia moja na kitu, deni la golikipa Rostand Tsh milioni 60 tumekuta deni la Ngoma, Obrey Chirwa mishahara yao George Lwandamina deni la Tsh milioni mia moja na kitu, tunataka watu wajue kwamba kipato tunachokipata ni kidogo kulinganisha na matumizi sababu,ninakiri kwamba wachezaji hawa miezi miwili hawajapata leo kama kila kitu kitaenda sawa leo jioni watapata pesa yao ya miezi miwilli”