SABABU YA REAL MADRID KUVAA JEZI ZA KIJANI NYUMBANI
Huenda ukastaajabu kuona Real Madrid wakiwa wamevaa jezi za kijani katika mechi yao ya nyumbani dhidi ya Espanyol kesho Jumamosi Santiago Bernabeu
Real Madrid watavaa jezi hizo kwa ishara ya kuunga mkono Mkutano wa umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya hali ya hewa ambao unafanyika jijini Madrid tangu Disemba 2 mpaka Disemba 16,2019
Hii itakuwa ni mara ya tatu Real Madrid kuvaa jezi za rangi hiyo msimu huu.
Mara ya kwanza walivaa katika mechi isiyo rasmi ya maandalizi ya msimu ambapo walicheza na Salzburg mwanzoni mwa mwezi Agosti Hazard akifunga goli lake la kwanza klabuni hapo. Baadae wakaja kuzivaa katika mechi ya ugenini dhidi ya Sevilla