UNAI BADO YUPO SANA ARSENAL
Baada ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Leicester City, klabu ya Arsenal sasa imekuwa na mwanzo mbaya zaidi katika kampeni yao kwenye ligi tokea msimu 1982/83.
Klabu hiyo tayari ipo nyuma ya vinara wa ligi kwa pointi 14, jambo kinaloonyesha klabu hiyo kuzidi kufanya vibaya tokea aondoke kocha Arsene Wenger.

Jambo hili limefanya mashabiki wa klabu hii kuzidi ongeza msukumo wa kocha huyu kufukuzwa ikiwa ni miezi 18 tokea ajiunge nao.
Kampuni nyingi za ubashiri hadi sasa zimemuweka mbele kocha huyu kama kocha anayeguatwa kutimuliwa.
https://twitter.com/David_Ornstein/status/1193459219292397568?s=19
Katika hali ya tofauti David Orstein mwandishi wa habari za uhakika za klabu hiyo na The Athletics wameeleza chanzo toka ndani ya klabu hiyo kimesema kuwa “Tupo nyuma ya Unai Emery kwa asilimia 100. Pia tunafikiria kusubiri hadi majira ya joto kabla ya kufanya maamuzi ya mbeleni.”

Chanzo hiki kimesema uongozi unaamini klabu ipo katika njia sahihi na wanaamini wakianza kupata matokeo mazuri hali itabadilika.