LEWANDOWSKI AENDELEZA MOTO WA MAGOLI
Mshambuliaji Robert Lewandoski ameendeleza rekodi yake ya ufungaji baada ya kufunga magoli mawili katika mechi ya Bayern Munich dhidi ya Borrusia Dortmund, mechi iliyoisha kwa Bayern kudhinda goli 4-0.
Lewandowski amekuwa ni mchezaji wa kwanza kufunga magoli 16 baada ya mechi 11 za mwanzo wa msimu wa Bundesliga huku akiwa amefunga katika mechi zote 15 katika mashindano yote akifunga jumla ya magoli 22.

Bayern sasa ipo katika nafasi ya 3 wakiwa na points zao 21 sawa na RB Leipzig waliopo katika nafasi ya 2 na nyuma kwa pointi 1 dhidi ya vinara Borussia Monchengladbach.