ZLATAN KUREJEA ACMILAN
Kamishina wa ligi ya soka ya Marekani MLS Don Garber amethibitisha mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic anayecheza katika klabu ya LA Galaxy ya Marekani,anawindwa na timu yake ya zamani AC Milan ya Italia.
Zlatan mwenye miaka 38 alijiunga na LA Galaxy mwaka 2018 na ameifungia magoli 53 hadi sasa akifanikiwa kutajwa katika kikosi bora cha ligi ya MLS msimu 2018-19, na mkataba wake na timu hiyo utamalizika mwishoni mwa mwaka huu.

Taarifa hii ya Zlatan kutakwa na AC Milan imethibitishwa na kamishina huyo wa MLS alipokuwa akizungumza na kituo cha ESPN.
“Zlatan ni mtu mzuri. Ananifanya niwe ‘busy’ sana na unahitaji aina hii ya wachezaji kama kile kilichotokea na Beckham miaka kadhaa iliyopita”
“Kwa sasa anawindwa na AC Milan, moja ya klabu kubwa duniani.” Alisema Garber wakati akiongea na ESPN. Zlatan aliichezea AC Milan kati ya waka 2010 na 2012 akiifungia klabu hiyo magoli 42 katika michezo 61 ya ligi.