BAADA YA KIPIGO TOKA KWA KAGERA SUGAR KMC YAMFUTA KAZI KOCHA WAO
Uongozi wa timu ya KMC ya Kinondoni leo hii wamefikia maamuzi ya kumfuta kazi kocha wao Jackson Mayanja raia wa Uganda baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu.
Maamuzi hayo yanakuja ikiwa saa chache zimepita toka timu hiyo ipoteze mchezo wa 4 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu dhidi ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1 mechi iliyochezwa uwanja wa uhuru DSM.