ALIYEMUIBIA MESUT OZIL ATUPWA JELA MIAKA 10
Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 30 anayefahamika kwa jina la Ashley Smith amehukumiwa miaka 10 jela kwa kosa la kufanya jaribio la unyang’anyi kwa wachezaji wawili wa Arsenal, beki wa kushoto Sead Kolasinac na kiungo Mesut Ozil.
Tukio hilo lilitokea mwisho mwa mwezi wa Julai mwaka huu huko nchini England ambapo Ashley Smith na mwenzake Jordan Northover waliwavamia wachezaji hao wakiwa kwenye gari wakijaribu kuwapora vito vyao zikiwemo saa za kifahari zenye thamani ya Pauni 200,000(Zaidi ya Tsh Milioni 500)

Kolisinac alipambana na wezi hao huku mchezaji mwenzake Mesut Ozil akibaki kwenye gari. Wezi hawa waliokuja wamebeba visu, walikimbia baada ya kushindwa kupambana na Kolasinac.

Smith,30, ambaye alielezewa na jaji wa mahakama Ian Bourne kuwa ni mtu mwenye matukio ya mengi ya uhalifu na anajulikana vizuri na polisi.