ZAHERA ADAI KUISAIDIA YANGA MILLIONI 100
Aliyekuwa Kocha mkuu wa Yanga SC Mwinyi Zahera baada ya kufutwa kazi na waajiri wake kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao ilivyo kwa sasa.
Zahera mbele ya waandishi wa habari aligoma kuongea kwa kigezo kuwa bado hajapewa barua lakini baada ya kupewa barua ameongea na kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM jinsi alivyojitoa na kueleza kuwa hakuona haja ya kufukuzwa.
“Hakuna hata siku moja nilitoa pesa nikasema Yanga mnirudishie tokea nilifika yanga? nimetoa pesa mingi inaweza fikia hata dola (usd) 50,000 yenye natia tu hivi bila ya kuomba wanirudishie, kwanza hata leo ukiangalia wachezaji siwezi waomba wanirudishie ,wachezaji walikuwa wanakuja kocha nitakurudishia nawapa milioni 2 mtu anafiwa”
Hadi anafukuzwa kazi Zahera ndani ya msimu huu 2019/20 ameifundisha Yanga katika michezo 10 akishinda michezo mitatu, sare michezo mitatu na amepoteza minne, toka April 24 2018 Zahera alipotua Yanga ameiongoza katika michezo 63, akishinda 32, amefungwa 21 na sare 10.