SAMATTA AIFUNGA LIVERPOOL, HALLAND AKIENDEA NA KUTUPIA MAGOLI
Mshambuliaji Mtanzania anayekipiga Genk jana alifunga goli lake la kwanza katika michuano hiyo ya Ulaya timu yake ikiambulia kipigo cha goli 2 – 1 toka kwa Liverpool. Liverpool walipata bao la kuongoza kupitia Georgino Wijnaldum dakika ya 14 kabla ya Mbwana Samatta kusawazisha dakika ya 40 kwa goli zuri la kichwa. Baada ya mapumziko Oxlade Chambelain dakika ya 53 aliipatia goli la ushindi Liverpool na kuifanya klabu hiyo kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa nyumbani msimu huu huku wakiwa wamefungwa mechi moja tu dhidi ya Napoli katika mashindano yote hadi sasa.
Liverpool sasa wamepanda na kuongoza kundi baada ya Napoli na Salzburg kutoa sare ya goli 1 – 1 mechi hiyo ikichezwa katika uwanja wa Napoli nchini Italia, mshambuliaji wa Salzburg Halland akiendeleza makali yake ya kutuoia magoli baada ya kufunga goli la mkwaju wa penati dakika ya 11 kabla ya Lozano kuja isawazishia Napoli dakika ya 43.