TFF IMEHITIMISHA SEMINA YA WAANDISHI 30 WA HABARI ZA MICHEZO KWA KUWAPA VYETI
Shirikisho la soka Tanzania TFF limefanikisha kufunga semina ya siku mbili ya waandishi wanawake wa habari za michezo Tanzania iliyokuwa inafanyika jijini Dar es Salaam.
Semina hiyo iliyokuwa inashirikisha waandishi wa habari za michezo 30 wanawake nchini Tanzania, ilikuwa na lengo la kuwaongezea zaidi maarifa waandishi hao na kuboresha uelewa wao katika tasnia hiyo.

Mmoja kati ya walimu wa Semina hiyo ni mwandishi raia wa Uganda Usher Komugisha anayefanya kazi na kituo cha Supersports cha Afrika Kusini.
Hii sio mara ya kwanza kwa TFF kuandaa semina hiyo kwani miezi miwili iliyopita pia ilifanya semina ya siku tano kwa waandishi 30 wa habari za michezo Tanzania