MANCHESTER UNITED YAANZA TENA KUPOTEZA
Hatua moja mbele, hatua mbili nyuma. Hicho ndicho kinazungumzwa sasa kuhusu Manchester United baada ya kupoteza mchezo wao ugenini dhidi ya Bournemouth.
United wanafika Vitality Stadium wakitafuta ushindi wa nne mfululizo katika michuano yote, lakini wanaondoka vichwa chini kwa kupoteza kwa goli 1-0 dhidi ya timu ambayo haikufunga goli kata moja mwezi Oktoba.

Zimwi likujualo, halikuli likakwisha. Ni Joshua King ambaye alikuwa Manchester United kwa muda wa miaka mitano (2009-2013),ndiye aliyekuwa muuaji wa leo kunako dakika ya 45, akitumia udhaifu wa kukaba wa Wan-Bissaka kufikisha mpira kwenye nyavu za David De Gea.

Manchester United imeshinda mechi moja tu kati ya 10 za mwisho walizocheza ugenini katika ligi kuu nchini England.