KOCHA AWEKA WAZI MSIMAMO WAKE AHOFII KUPOTEZA AJIRA YAKE YANGA
Yanga SC ikiwa inaelekea katika mchezo wa mwisho wa kupambania nafasi ya kucheza Kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids utakaochezwa Novemba 3 2019 Cairo katika uwanja wa 30 June, kocha wao Mwinyi Zahera akifanya mahojiano na Clouds Plus ameweka wazi msimamo wake kuwa haogopi kupoteza nafasi yake hiyo Yanga, kwakuwa yeye ni kocha anaweza kuondoka na kwenda kufanya kazi popote tu sio lazima tu iwe Yanga.
“Katika maisha yangu hakuna walipoandika kuwa Zahera utafia Yanga, hapana mimi ni kocha leo niko hapa kesho nitakuwa sehemu nyingine mimi naweza kutoka Yanga hata bila kufukuzwa” alisema Zahera katika mahojiano maalum na Clouds Plus
Kocha Zahera hivi karibuni alikutana na wakati mgumu baada ya Yanga kupoteza nyumbani katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza 2-1 dhidi ya Pyramids na baada ya mchezo mashabiki wanaoaminika kuwa wa Yanga walimtolea lugha za matusi na kumrushia chupa za maji.