KIZUGUTO WA TFF AULA CAF, KWENDA KUWA MRATIBU WA AFCON -23
Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limetangaza rasmi kumchagua Baraka Kizuguto kutoka shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuwa miongoni mwa waratibu wasaidizi wa AFCON U-23.
Kizuguto ametangazwa rasmi kuwa atakuwa mratibu (AGC) wa mashindano ya mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa miaka 23 (AFCON U-23) yatakayochezwa nchini Misri kwa siku 14.
Michuano hiyo itakayochezwa Cairo nchini Misri inatarajiwa kuanza Novemba 8 2019 hadi Novemba 22 2019 yaani itikishirikisha jumla ya mataifa 8 (Misri, Cameroon, Mali, Ghana, Nigeria, Ivory Coast, South Africa na Zambia).