KAWHI LEONARD AWAADHIBU WAAJIRI WAKE WA ZAMANI
Baada ya jana kupoteza ugenini dhidi ya Utah Jazz, Los Angels Clippers leo wamerejea katika uwanja wao wa nyumbani Staple Center na kuibuka na ushindi dhidi ya San Antonio Spurs.
Clippers leo wameshinda kwa pointi 103-97, huku nyota wao Kawhi Leonard akiibuka nyota wa mchezo, akifunga Pointi 38, Rebounds 12 dhidi ya timu yake ya zamani.

Mpaka sasa Clippers ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa msimu huu, wameshinda mechi nne wakipoteza mbili, na kesho wanayo nafasi ya kulipa kisasi dhidi ya Utah Jazz katika uwanja wao wa nyumbani Staples Center.