GRANIT XHAKA AVUNJA UKIMYA BAADA YA KITENDO CHAKE DHIDI YA CRYSTAL PALACE
Nahodha wa Arsenal Granit Xhaka hatimaye amefunguka kuhusiana na kilichotokea baada ya kuzomewa na mashabiki wa Arsenal huku Xhaka akionesha lugha ya ishara inayoashiria kubeza kuzomewa huko.
Xhaka alifanyiwa mabadiliko katika mchezo wa Ligi Kuu England Jumapili iliyopita kati ya Arsenal dhidi ya Crystal Palace uliyochezwa katika uwanja wa Emirates na kumalizika kwa sare ya kufungana 2-2.

Wakati anafanyiwa mabadiliko hayo dakika ya 61 na kuingia Bakayo Saka, Granit Xhaka akiwa anatoka alizomewa na mashabiki wa Arsenal na kuvua kitambaa cha unahodha na kukirusha juu pamoja na kutupa jezi yake akielekea katika vyumba vya kubadilishia nguo huku akidaiwa kutoa lugha ya tusi “f*** off”
Baada ya mchezo kocha wa Arsenal Unai Emery alitaka Xhaka aombe radhi kwa kitendo hicho na jana Alhamisi Xhaka aliamua kuandika na kueleza mkasa mzima baada ya kuwa kimya kwa siku nne.
https://www.instagram.com/p/B4S0q45HTAL/?utm_source=ig_web_button_share_sheet“Baada ya kuchukua muda kutafakari kilichotokea Jumapili mchana, ningependa kutoa ufafanuzi kuliko kukaa kimya kabisa, kitendo cha kufanyiwa mabadiliko kiliniondoa kabisa, naipenda hii klabu na siku zote nitajitoa kuitumikia kwa asilimia 100 ndani ya uwanja na nje ya uwanja”
“Hisia zangu hazikueleweka kwa mashabiki na kurudiwa maneno ya kinyanyasaji wakati wa mchezo na katika mitandao ya kijamii na wakisema maneno ‘tutakuvunja miguu’ ‘tutamuua mkeo’ ‘tunatamani mwanao apate kansa’ . Hivyo vilinichochea.
Sikuwa na nia mbaya na samahani kama watu walinifikiria tofauti” alisema mchezaji huyo kupitia taarifa rasmi ambayo aliiweka kwenye mtandao wa kijamii.