VERSTAPPEN APOKWA ‘POLE POSITION’ BAADA YA KUPIGWA PENATI
Akiwa amedhamiria kutafuta ushindi katika mbio za Mexican Grand Prix, hali inaonekana kutokuwa shwari kwa Maxi Verstappen baada ya kupigwa penati ya nafasi tatu na hivyo kuondoka katika ‘pole position’. Sasa Vertappen ataanzia katika nafasi ya nne nyuma ya Charles Leclerc, Sebastian Vettel, Lewis Hamilton na mbele ya dereva mwenza Alexander Albon anayeanzia katika nafasi ya tano.

Hii ilikuwa ‘pole position’ ya pili kwa Verstappen msimu huu ya kwanza ikiwa mwezi Agosti katika Hungary Grand Prix. Penati hii amepigwa kwa kosa la kutopunguza mwendo kwenye tahadhari ya kibendera cha njano baada ya Valtteri Bottss kupata ajali.

Sasa dereva huyu wa RedBull leo ana kazi ya kushindana na madereva wa Ferrari waliopo mbele yake ambao wapo na faida ya kuwa na gari zenye kasi kwenye njia zilizonyooka huku akiwa na kazi nyingine ya kupambana na Lewis Hamilton amabaye anapambania kimaliza katika nafasi za juu mbali na dereva mweza Valtteri Bottas na kuifanikiwa kuibuka bingwa wa Dunia.