PATRICK AUSSEMS AJIVUNIA KAGERE NI BAADA YA KUENDELEZA MOTO VPL
Mshambuliaji wa Kinyarwanda Meddie Kagere anayekipiga Simba SC licha ya baadhi ya watu kumtania na kusema ana umri mkubwa lakini ameendeleza balaa uwanjani kwa kuwa anafunga karibia kila mchezo.
Kagere akiichezea Simba SC katika mchezo dhidi ya Azam FC walioshinda 1-0 kwa goli lake pekee la dakika ya 49, hilo linakuwa ni goli lake la 7 VPL msim huu akiwa kacheza mechi 5 ni wastani wa kufunga goli kila baada ya dakika 64.
Kocha wa Simba SC Patrick Aussems ameonesha kumwagia sifa mchezaji huyo na kwa kutoa kauli kuwa Meddie Kagere anahitaji mpira tu ili afunge na sio vinginevyo, kauli ambayo inaonesha kujivunia kwake kuwa na mchezaji huyo.

“Sisi (Simba) tunacheza kitimu kuhusu Meddie Kagere kufunga !!! anahitaji mpira mzuri tu kama utakubaliana na mimi, ukimuweka Meddie peke yake hatokuwa na uwezo wa kufunga lakini kama anakuwa na mchezaji mwingine wa kumpa mipira mizuri anafunga, unajua Meddie ni muuaji anapata nafasi moja na kufunga ni kitu kizuri kwake na timu kwa ujumla” alisema Aussems baada ya mechi.
Simba wanaendelea kuongoza ligi hiyo wakiwa wameshinda mechi zao zote tano walizocheza msimu huu katika VPL.