DAKIKA 15 ZIMEMTOSHA PEPE KUWA SHUJAA WA ARSENAL KATIKA UWANJA WA EMIRATES
Baada ya kuibuka gumzo mitandaoni na kukosolewa kutokana na kudaiwa kukosa goli la wazi katika mchezo wa EPL dhidi ya Sheffield timu yake ya Arsenal ikipoteza 1-0, Nicholas Pepe anawafunga watu midomo.
Usiku wa Europa League kocha wake Unai Emery aliamua kumuanzishia benchi Nicolas Pepe katika mchezo dhidi ya Vitoria ambao ulimalizika Arsenal kwa kupata ushindi wa 3-2.

Pepe aliingia dakika ya 75 akitokea benchi kuchukua nafasi ya Lacazette wakati ambao Arsenal walikuwa nyuma 2-1 , Pepe baada ya kuingia dakika ya 80 akafunga goli la kusawazisha watu wakiwa wanaamini kuwa mechi inaisha sare dakika ya 90 Pepe akafunga goli la ushindi kwa Arsenal.Magoli hayo yote alifunga kwa ‘Freekick’

Goli la kwanza la Arsenal lilifungwa na Martinelli dakika ya 32 wakati Magoli ya Vitoria Guimaraes yakifungwa na Edwards dakika ya 8 na Bruno Duarte dakika ya 36 .
Arsenal sasa inaongoza kundi lake kwa alama 9 huku Vitoria wakishika mkia kwa kuwa na alama 0.