AYEW AFUNGUKA MAUZA UZA YA CHAMA CHA SOKA GHANA (GFA)
Mshambuliaji wa Swansea City ya England Andrew Ayew ambaye pia ni nahodha wa Ghana ameeleza kusikitishwa na chama cha soka nchini Ghana GFA kwa kushindwa kuandaa michezo ya kirafiki ya kimataifa wakati wa mapumziko ya mechi za kalenda ya FIFA.
Nyota huyo anaamini kama kungekuwepo kwa michezo ya kirafiki anaamini ingesaidia maandalizi ya mchezo wao wa kuwania kufuzu AFCON 2021 Novemba 15 Accra dhidi ya Afrika Kusini wakifuatiwa na mechi dhidi ya Sao Tome Novemba 19.

“Tunahuzunika kwa sababu hatujacheza michezo ya kirafiki na hatujui kwa nini, tulianza vizuri kweli 2014 kwa kucheza michezo ya kirafiki na mataifa makubwa kama Urusi licha ya kuwa tulikuwa na matatizo kidogo, toka kipindi hicho tumelipoteza shirikisho letu” alisema Ayew kupitia mtandao wa Modern Ghana
“Tumesikitishwa sana kwa sababu katika madirisha mawili ya mechi ya kimataifa yaliyopita , hatujacheza mechi yoyote ya kirafiki na hatujui kwa nini” alisema mshambuliaji huyo

Chama cha soka cha Ghana kimeshindwa kuandaa michezo ya kimataifa ya kirafiki kwa kukumbwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kuishiwa pesa kwenye akaunti za GFA.
Ghana ilishindwa kufuzu michuano ya kombe la Dunia mwaka 2018, na mwaka huu kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 11 wameshindwa kufuzu hatua ya nusu fainali katika michuano ya AFCON.