DENIS ONYANGO AENDA KUMZIKA BABA YAKE, HUENDA AKAWAKOSA KAIZER CHIEFS
Klabu ya Mamelod Sundowns huenda ikamkosa kipa wao Denis Onyango katika mchezo mgumu ligo dhidi ya Kaizer Chiefs Jumapili hii kufuatia kumruhusu kipa huyo kwenda nyumbani kwao Uganda kujumuika na familia kwa maziko ya baba yake mzazi.
Mzee Gabriel Onyango ambaye ni baba mzazi wa kipa huyo amefariki kwa kansa, hivyo Onyango amebidi aruhusiwe kurudi Uganda kuzika wakati zikiwa zimesalia siku nne kuelekea Oktoba 27 kucheza dhidi ya Kaizer Chiefs.
Onyango amekosekana katika mchezo wa jana Jumatano dhidi ya Higlands Park inayochezewa na mtanzania Abdi Banda ambapo Mamelod walipata ushindi wa goli 1-0.
Mamelod kwa sasa wapo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini wakiwa na alama 17 dhidi ya Kaizer Chiefs anayeongoza kwa alama 19 huku akiwa mbele mchezo mmoja