MICHAEL WAMBURA KAFAIDIKA NA MSAMAHA WA RAIS MAGUFULI SASA HURU
Aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho la mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini TFF Michael Richard Wambura leo ameachiwa huru katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Wambura ameachiwa huru baada ya kukubali kutii agizo la Rais Magufuli la wale waliokuwa wanatuhumiwa kwa kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi kupitia kwa DPP kama watakiri na kurudisha pesa wanazotuhumiwa nazo wataachiwa huru.
Baada ya Wambura kukiri kosa na kukubali kurejesha Tsh milioni 100 alizokuwa anatuhumiwa nazo katika makosa yake, atalipa pesa hizo kwa awamu tano na leo ameachiwa baada ya kulipa Tsh milioni 20 mbele ya hakimu mfawidhi Kelvin Mhina, maamuzi hayo yakiwa yanakuja ikiwa ni miezi 7 na siku 26 toka afikishwe Mahakamani kwa mara ya kwanza Februari 11 2019.