REAL MADRID TIA MAJI TIA MAJI LIGI YA MABINGWA
Hadi sasa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ikiwa na kocha wake Zinedine Zidane haijashinda mchezo wowote wa Ligi ya Mabingwa msimu huu baada ya kucheza michezo miwili ya makundi.
Mchezo wao wa kwanza walipoteza 3-0 dhidi ya PSG kabla ya mchezo wao wa pili wa leo dhidi ya Club Brugge kutoka sare ya 2-2 wakitokea nyuma kwa mabao mawili.

Real Madrid ndani ya dakika 39 walikuwa wameruhusu magoli mawili yaliofungwa na Emmanuel Dennis dakika ya 9 na 39, Dennis alikuwa kaahidi akifunga goli Bernabeu katika mchezo huo atachora tattoo ya ukumbusho.
Hiyo inatokana na ukubwa wa klabu ya Real Madrid, uimara wake lakini na ubora wao wa kihistoria wa kutawala michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kukiwa hakuna timu yoyote iliyowahi kutwaa taji hilo mara nyingi zaidi ya Real Madrid.

Jitihada za wachezaji na mabadiliko ya mlinda mlango Thibaut Courtois na kuingia Alphonse Areola kulionekana kuimarisha safu ya ulinzi na Real Madrid kufanikiwa kusawazisha kwa magoli ya Sergio Ramos dakika ya 55 na Casemiro dakika 85 na kuifanya Real Madrid ivune alama moja ikiwa ndio ya kwanza kwao msimu huu katika michuano hiyo.