KUTOKA FAINALI YA UEFA 2018/19 HADI KIPIGO CHA KIHISTORIA
Wengi hawaamini Tottenham Hotspur wanayumba na nini ukizingatia msimu uliopita walikuwa bora katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kiasi cha kufanikiwa kufikia hatua ya fainali ya michuano hiyo na kucheza dhidi ya Liverpool.

Spurs wamepigwa kipigo cha kihistoria 7-2 kutoka kwa FC Bayern Munich ikiwa ndio kipigo chao cha kwanza kikubwa nyumbani katika historia mechi za nyumbani za mashindano toka klabu hiyo ianzishwe 1882.

Safu ya ushambuliaji ya Bayern ilikuwa On fire baada ya Joshua Kimmich kufungua njia kwa bao la dakika ya 15 nae Lewandowski akaja kutupia mawili dakika ya 45 na 87 huku shujaa wa mchezo huo Serge Gnabry kufunga hart-trick akipiga mabao mannne dakika 53, 55, 83 na 88 huku bao la dakika ya 12 la Son Heung-min la mkwaju wa penati la Harry Kane dakika ya 61 yakiwa hayana msaada.