JOSEPH PARKER ATOLEWA KATIKA PAMBANO LAKE NA CHISORA
Bingwa wa zamani wa uzito wa juu Joseph Parker ameondolewa katika pambano lake na Dereck Chisora ikiwa zimebaki wiki chache kufanyika.
Pambano hilo lilipangwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu.
Taarifa kutoka kwa promota Eddie Hearn imeeleza Parker,27, atashindwa kushuka katika pambano hilo kutokana na kuwa mgonjwa.
“Tunafanya kazi kuona tunapata mbadala sahihi na tutaleta taarifa zaidi wiki hii.” alisema Eddie Hern

Pambano hili linaonekana kuingiliwa na vikwazo kwa mara nyingine baada ya mwezi uliopita Chisora, 35, kutoa maneno makali katika mkutano wa wandishi wa habari kuonesha kutopendezwa na pambano lake kuwa la utangulizi na huku akidai pambano kuu lile la Josh Taylor dhidi ya Regis Prograis ndio liwe la utangalizi kwa sababu hawafahamiki.