ALAN RUSCHEL AFUNGA GOLI LA KWANZA BAADA YA KUNUSURIKA KWENYE AJALI YA NDEGE ILIYOUA WATU 71
Ajali ya ndege ya LaMia 2933 iliyokuwa imebeba wachezaji wa klabu ya soka ya nchini Brazil ya Chapecoense iliyotokea Novemba 28 2016 ni moja kati ya matukio kubwa la kihistoria katika soka toka karne ya 21 ianze.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 77 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na wahudumu wa ndege wakitoka Brazil kwenda Colombia katika mchezo wa fainali wa Klabu Bingwa Amerika Kusini (Sudamericana) na walinusurika sita kati ya 77 akiwemo mchezaji Alan Ruschel.

Ruschel ,30, ndio miongoni mwa manusura waliopona na kufanikiwa kurejea uwanjani kucheza soka tena Agosti 7 2017 lakini ilimchukua muda mrefu kufunga goli hadi Septemba 30 2019 akifunga bao la ushindi 1-0 dhidi ya Cruzerio akiichezea Goias kwa mkopo akitokea Chapecoense aliyokuwa nayo wakati inapata ajali katika kijiji cha Cerro Gordo nchini Colombia