REAL MADRID BADO WANAENDELEA NA REKODI LALIGA 2019/20
Klabu ya Real Madrid baada ya kuwa wageni wa ndugu zao wa jiji la Madrid klabu ya soka ya Atletico Madrid katika uwanja wa Wandametropolitan, imejikuta ikifanikiwa kuendelea na rekodi yake ya LaLiga msimu huu baada ya kutokubali kupoteza.
Real Madrid ikiwa ugenini imefanikiwa kuvuna alama moja katika mchezo wa sare tasa (0-0) dhidi ya wapinzani wao wakuu (Madrid Derby), mchezo huo ni mchezo wa 7 wa Real Madrid katika Ligi Kuu Hispania LaLiga na haijapoteza hata mmoja na kuwa klabu pekee LaLiga ambayo haijapoteza mchezo msimu huu.

Sare hiyo imeifanya Real Madrid kuendelea kuongoza msimamo wa LaLiga wenye jumla ya timu 20, Real anaongoza kwa kuwa na alama 15, akicheza michezo 7, sare 3 na ushindi michezo 4, Atletico wao wapo nafasi ya 3 kwa kuwa na alama 14, akicheza michezo 7 na ushindi michezo 4, sare 2 na wamepoteza mchezo mmoja.