LAMPARD KAHOJI LEEDS NA KOCHA WAO KUPEWA TUZO YA FAIR PLAY
Kocha wa klabu ya Chelsea ya nchini England Frank Lampard amehoji maamuzi ya FIFA kuamua kuipa klabu ya Leeds United na kocha wake Marcelo Bielsa tuzo ya Fair Play katika tuzo za Fifa The Best zilizofanyika mwanzoni mwa juma jijini Milan Italia.
Lampard anahoji na kusema kuwa Marcelo na timu yake hawakupaswa kushinda tuzo ya Fair Play mwaka huu ambao walikuwa katika kashfa ya kuwatuma staff wake wakaipeleleze Derby County aliyokuwa anaifundisha (Lampard) wakati huo na baadae kocha Marcelo Biesla kukiri kufanya hivyo na Leeds kupigwa faini ya Pauni 200,000.
Frank Lampard anasema alitabasamu baada ya kuona Leeds na Biesla wameshinda Tuzo hiyo, alisema kocha huyo kuelekea mechi dhidi ya Brighton jana.
“Tunawajua wanaopiga kura kwa ajili ya hivi vitu.?!
Kupata tuzo ya Fair Play (licha ya kashafa hiyo ya upelelezi), nilidhani ni kejeli. Yalikuwa maamuzi ya ajabu kwa wao kushinda tuzo hiyo. Ninadhani kila mmoja alikuwa na mshangao huo”. Alisema Lampard
Leeds na Marcelo Biesla walipata tuzo hiyo baada ya kuonesha kitendo cha kiungwana katika mechi yao dhidi ya Aston Villa msimu uliopita.
Leeds waliwaachia Aston Villa wakasawazishe goli baada ya wao kufunga goli wakati mchezaji wa Aston Villa Jonathan Kodjia akiwa amelala chini baada ya kuumia.