CHARLES LECLERC ACHUKUA ‘POLE POSITION’ MARA YA 4 MFULULIZO
Katika mbio za Russian GP dereva wa Ferrari Charles Leclerc kesho ataanza katika “pole position” ikiwa ni mbio za nne mfululizo kufanya hivi. Hii ni mara ya kwanza kwa dereva kuchukua ‘pole position’ katika mbio nne mfululizo toka Lewis Hamilton afanye hivi mwishoni mwa msimu wa 2016. Pia ni dereva wa kwanza wa Ferrari kufanya hivi tokea Michael Schumacher 2001.
Baada ya mbio, Hamilton aliwasifia Ferrari huku akieleza hawakutegemea kumaliza katika nafasi za juu kutokana na Ferrari kuwa wazuri katika spidi katika barabarani.
Leclerc amemaliza mbele ya Lewis Hamilton na dereva mwenza Sebastian Vettel hii ikiwa ni mara ya 9 mfululizo anamaliza mbele yake. Verstapen wa RedBull amemaliza katika nafasi ya nne mbele ya Bottas wa Mercedese.
Russian GP iliyopita Hamilton alifanikiwa shinda na kuzidi kujikita kileleni dhidi ya mpinzani wake Sebastian Vettel katika mbio za kuwania ubingwa wa dunia.