MASHABIKI WATOA SABABU YA KUONESHA BANNER YA HAZARD KATIKA MECHI NA LIVERPOOL
Baada ya miaka 7 ndani ya jezi ya bluu, Eden Hazard ameondoka na kujiunga na Real Madrid katika majira ya kiangazi mwaka huu kwa ada ya Pauni Milioni 130.
Jana katika dimba la Stamford Bridge, Chelsea waliikaribisha Liverpool katika mchezo wa ligi kuu nchini England, kitu cha kustaajabisha ni mashabiki wa Chelsea kuionesha banner ya Eden Hazard kabla ya mchezo huo.
Kitu hicho kiliwashangaza wengi wakihoji sababu ya banner ya mchezaji huyo kuoneshwa kabla ya mchezo huo.
Taarifa kutoka ukurasa mmoja wa mashabiki wa Chelsea ilieleza kuwa Banner hiyo ya Eden Hazard ilitoka kimakosa bila ya kujua.
.
“ Watu kiukweli wanafikiri bendera ya Hazard ilitumika kwa kudhamiria katika jukwaa la Matthew Harding. Ile ilikuwa ni makosa.
Kuna kazi kubwa inafanyika katika kuratibu vitu hivi na kuna bendera nyingi, ilikuwa lazima kutokea siku moja” uliandika ukurasa huo wa mashabiki wa Chelsea, unaoitwa We Are The Shed.