MAN UNITED YAMSIKITISHA JOSE MOURINHO
Kocha Jose Mourinho amesema timu ya Man United ya sasa ni mbovu zaidi ya ile ya msimu uliopita.
Jose amesema hayo jana wakati anachambua mechi ya West Ham na Man United katika studio za Sky Sports.
Jose alipoulizwa kama United wataweza kuzifikia timu mbili za juu katika ligi, alijibu “ Wapo mbali. Mimi si mtu sahihi kujibu hili swali. Ni vigumu kujibu.
.
‘Nimekuwa pale kwa misimu miwili ambapo niliweza kuona vitu vingi vizuri na kuweza kuona mwelekeo wa kwenda. Msimu wa tatu haukuwa mzuri. Nikafukuzwa, pengine nilistahili kufukuzwa kwa sababu mimi ndio mtu wa mwisho kuwajibika kama Meneja.”
.
‘Lakini kwa ukweli unaouma ni kwamba (Man United) ni wabaya kuliko kabla. Na kwangu mimi ni kitu cha huzuni. Labda watu wanafikiri ninafurahia hali hii,lakini sifurahii kiukweli.’ Amesema kocha huyo.
Jose ambaye alifukuzwa United mwezi Disemba mwaka jana, amesema timu hiyo ipo katika matatizo makubwa na sio tu watapata shida kuingia nne bora, bali hata kuingia sita bora.