VALVERDE ROHO JUU!! BARCELONA IKIINGIA REKODI MBOVU KWA MARA YA KWANZA BAADA YA MIAKA 25
Kocha wa Barcelona ya nchini Hispania Ernesto Valverde anazidi kupata presha baada ya kiwango kibovu cha timu yake kilichopelekea kupoteza mchezo wao wa pili wa LaLiga dhidi ya Granada iliyopanda daraja kwa bao 2-0.
Barcelona inaonekana kuwa chini ya kiwango kwani kuna baadhi ya takwimu nadra kuzikutaka zikitokea kwa Barcelona, hadi dakika ya 67 ya mchezo huo Granada walikuwa na mashuti manne yaliolenga lango na Barcelona wakiwa hawana hata moja kitu ambacho ni presha zaidi kwa Valverde.
Mabao ya Ramon Azeez dakika ya pili na Alvaro Vadillo kwa mpira wa adhabu ya penati dakika ya 66, inaiingiza Barcelona katika rekodi mbaya, Barcelona baada ya kipigo hiko inakuwa katika rekodi ya kutoshinda ugenini toka mwezi April mwaka huu katika LaLiga.
Barcelona ikicheza mchezo wake wa tatu wa LaLiga ugenini msimu huu imeambulia kuvuna alama moja tu kati ya tisa, Barcelona wanashindwa kupata matokeo mazuri katika michezo 7 mfululizo msimu katika mashindano yote, hii ndio mara ya kwanza Barcelona kuwa na mwanzo mbovu katika Ligi baada ya miaka 25 (1994-1995).