SEBASTIAN VETTEL NA FERRARI WAWASHANGAZA MERCEDESE SINGAPORE GRAND PRIX
Siku 392 ndizo alizokaa bingwa wa dunia mara 4 Sebastian Vettel wa timu ya Ferrari bila ya kushinda mbio zozote ukiwa ni muda mrefu zaidi kwake bila ushindi huku akionekana kuishi katika kivuli cha dereva mwenza Charles Leclerc ambaye wengi walitegemea awe chini yake ila amekuwa akifanya vyema zaidi kuliko ilivyotegemewa akishinda mbio mbili mfululizo na kuwa dereva aliyeanza katika Pole position mara nyingi kuliko mwingine yeyote yule msimu huu, mara tano.

Vettel na timu yake ya Ferrari walifika Singapore bila matarajio makubwa huku wakiwa hawapewi nafasi tofauti na timu hasimu ya Mercedes iliyopewa nafasi ya kushinda mbio hizi ikiongozwa na nyota Lewis Hamilton na dereva mwenza Valtteri Bottas.

Hali haikuwa kama matarajio ya wengi kwani mbio hizi zimeisha kwa kishindo kwa dereva Sebastian Vettel kuandikisha ushindi wake wa 53 na wa 5 kwa Singapore Grand Prix ukiwa ni ushindi wake wa kwanza baada ya kumaliza mwaka mzima bila ushindi, ushindi ambao aliutoa kwa mashabiki wake waliomtia moyo na kumpa sapoti katika kipindi chote. Pia ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Ferrari hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza tokea mwaka 2008.

Charles Leclerc amemaliza katika nafasi ya pili mbele ya Max Vesterppen wa RedBull huku nyota Lewis Hamilton akimaliza katika nafasi ya 4 mbele ya dereva mwenza Valtteri Bottas. Alexander Albon wa RedBull ameendelea weka juhudi akimaliza katika nafasi ya sita mbele ya Lando Norris wa Renault.

Msimamo wa maderva kwa sasa anaongoza Lewis Hamilton mwenye points 296 akifuatiwa na Bottas points 232, nafasi ya 3 Charles Leclerc points 200 sawa na Max Verstappen huku nafasi ya 5 ikishikwa na Sebastian Vettel mwenye points 194.

Mbio zijazo ni Russian Grand Prix weekend ijayo ambazo msimu uliopita ziliisha kwa Bottas kumwachia Hamilton ampite nakuchukua nafasi ya kwanza iyokuwa amalize yeye yakiwa ni melekezo ya moja kwa moja toka kwa uongozi wa timu mkakati uliokuwa unamsaidia Hamilton kuweza jiweka kileleni kwa points 50 mbele ya hasimu wake Sebastian Vettel katika mbio za kushinda ubingwa wa dunia. Kwa kijana Charles Leclerc aliyekuwa anashiriki kwa mara ya kwanza mbio hizo alimaliza katika nafasi ya 7 na timu yake ya Sauber Alfa Romeo.
