LAMPARD AELEZEA HALI YA MASON MOUNT NA HOFU YAKE KWA KANTE
Kukiwa tunaelekea kutazama mchezo wa 184 Jumapili hii ya Septemba 22 wa timu za Liverpool na Chelsea kuwahi kukutana toka Desemba 25 1907 walipokutana mara ya kwanza, kocha mkuu wa Chelsea Frank Lampard ametoa taarifa za majeruhi.
Kufuatia kutolewa dakika ya 16 ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa Mason Mount huku Chelsea ikipoteza 1-0 nyumbani dhidi ya Valencia, Lampard amethibitisha kuwa Mount aliyetolewa kwa kupata jeraha la kifundo cha mguu ana nafasi ya kucheza mchezo huo wa jumapili kwa maana anaendelea vizuri.

Lampard ameeleza Mount yuko fiti kama ilivyo kwa N’golo Kante ambaye kwa upande wake anaona yupo sawa ila anakosa utimamu wa mechi (game fitness).
Chelsea kesho Jumapili wapo nyumbani Stamford Bridge kuwakaribisha vinara wa ligi Liverpool, mchezo huo utachezwa kuanzia saa 12:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki