CHARLES LECLERC KUANZA KATIKA ‘POLE POSITION’ SINGAPORE GRAND PRIX
Dereva wa Ferrari Charles Leclerc, 21, amefanikiwa kuongoza katika mbio za kufuzu Singapore Grand Prix hivyo ataanza katika nafasi ya kwanza hapo kesho.
Dereva huyo amemaliza mbele ya Lewis Hamilton kwa sekunde 0.191 na dereva mwenza Sebastia Vettle kwa sekunde 0.2 huku Max Verstappen wa Redbull akimaliza katika nafasi ya nne mbele ya dereva mwenza Alexander Albon.

Matokeo haya yamekuja kwa kushangaza baada ya timu ya Ferrari kuonekana kusuasua katika Practice jana Ijumaa kutokana na mbio hizi kuwa na kona nyingi na kuhitaji matumizi ya tairi laini hali ambazo zimekuwa zikiwaondoa Ferrari katika ushindani.
Hii ni mara ya tatu mfululizo Charles Leclerc anashinda Pole Position na ni mara ya tano kwa msimu huu inayomfanya kuwa dereva aliyeanza katika nafasi hiyo kwa mara nyingi zaidi mbele ya Bottas na Hamilton wote walioanza mara 4.