LIVERPOOL WALIFURAHI KUMUUZA FERANANDO TORRES KWENDA CHELSEA 2011
Jamie Carragher amesema kuwa yeye pamoja na wachezaji wenzake wa Liverpool, walifurahi kuona Fernando Torres anaihama timu hiyo na kwenda Chelsea kwa sababu kiwango chake kilikuwa tayari kimeisha.
Torres aliondoka Liverpool mwaka 2011 na kujiunga na Chelsea kwa ada ya Pauni Milioni 50 na kuweka rekodi mpya ya usajili nchini England na kuwa mchezaji ghali wa sita katika historia ya soka.
.
“Hatukutaka kuzuia Torres kujiunga na Chelsea” Carragher aliiambia Sky Sports
.
“Muda wake (wa kung’aa) ulikuwa umeisha. Pauni Milioni 50 zilikuwa nyingi sana, hatukuamini.
Nilishitushwa na pesa zilizolipwa”
.
Maisha ya Fernando Torres katika klabu ya Chelsea hayakwenda vizuri na kupelekea kutolewa kwa mkopo kwenda AC Milan mwaka 2014 na baadae kujiunga moja kwa moja.
Carragher anasema kocha wa Chelsea wa kipindi kile Carlo Ancelotti alifanya makosa kwa kumchezesha Torres katika mechi dhidi ya Liverpool, ikiwa ndiyo mechi yake ya kwanza kuichezea Chelsea.
Carragher anaamini Torres kuchezeshwa katika mechi hiyo iliyoisha kwa Chelsea kufungwa goli 1-0,ilichangia kuharibu maisha yake yote klabuni hapo.