BIRMINGHAM CITY WAPIGWA FAINI YA MILIONI 121,SHABIKI WAO AKIFUNGIWA MIAKA 10
Klabu ya Birmingham City imepigwa faini ya pauni 42,500 (Tsh Milioni 121) na chama cha soka cha England FA kwa kosa la shabiki wake kuvamia na kuingia uwanjani na kumshambulia mchezaji wa Aston Villa Jack Grealish mwezi March 10 katika uwanja wao wa ST Andrew.
Shabiki huyo anayetambulika kwa jina la Paul Mitchell ,27, baada ya kufanya kosa hilo alihukumiwa wiki 14 gerezani sambamba na kufungiwa kwa miaka 10 kutoingia katika viwanja vyote vya soka.
Mitchell aliingia uwanjani dakika ya 10 ya mchezo huo wa Birmingham na Aston Villa na kumvuta kwa nyuma Jack Grealish.
Baadae shabiki huyo akatolewa uwanjani na wachezaji wa timu zote mbili pamoja na mlinzi wa uwanjani.