MURRAY AWEKA REKODI US OPEN
Jamie Murray ndugu wa Andy Murray amefanikiwa kuweka rekodi ya kuwa mwanaume wa kwanza kutwaa taji la US Open Mixed Double kwa mwaka wa nne mfululizo hii ikiwa ni Grand Slam yake ya 7 na kwa Bethanie Mattek-Sands ikiwa ni Grand Slam yake ya 9 kwa mashindano ya double.
Jamie alicheza kwa pamoja na Mmarekani Bethanie Mattek-Sands na kufanikiwa kutetea ubingwa wao baada ya kushinda kwa seti 6-2 6-3 dhidi ya Chan Hao-ching aliyecheza kwa pamoja na Michael Venus.
Katika michuano hii Murry pia alikuwa akicheza Double kwa upande wa wanaume kwa pamoja Skupski na kutolewa katika hatua ya nusu fainali.