NAOMI OSAKA ATOLEWA KATIKA US OPEN 2019
Baada ya bingwa mtetezi wa US Open kwa upande wa wanaume Novak Djokovic kutolewa katika michuano hiyo hapo jana, leo bingwa mtetezi kwa upande wa wanawake Naomi Osaka nae amefuata njia ile ile.

Osaka,21, ametolewa katika raundi ya nne ya michuano hiyo kwa kufungwa seti 7-5,6-4 na mwanadada Belinda Bencic,22, kutoka nchini Switzerland.
Naomi Osaka ambaye alipata maumivu ya goti wiki mbili zilizopita, anapoteza mechi dhidi ya Bencic kwa mara ya tatu mfululizo mwaka huu.

Sasa Osaka atapoteza nafasi yake ya kwanza kwenye viwango vya ubora na Ashleigh Barty wa Australia kurejea katika nafasi hiyo.