KINDA COCO GAUFF KUKUTANA NA BINGWA NAOMI OSAKA
Akiwa anashiriki kwa mara ya pili mashindano ya grand slam, kinda Coco Gauff mwenye umri wa miaka 15 atakutana na bingwa mtetezi Naomi Osaka katika raundi ya tatu kwenye US Open.

Ni moja ya mechi zinazotazamiwa kuwa na mvuto huku kinda huyo aliyeshinda taji lake la kwanza la WTA double Washington Open akimwagiwa sifa za kutosha na magwiji Serena Williams na Roger Federer kama hazina nzuri kwa mchezonwa tenis siku za usoni.

Mechi nyingine itakuwa kati ya mwanadada Caroline Wozniacki dhidi ya Biassca Andreescu aliyeshinda taji lake la pili WTA mapame mwezi huu baada ya William kushindwa endelea na mechi huku akiwa anaingia na kumbukumbu nyingine nzuri ya kumfunga mkali mwingine Mjerumani Angelique Kerber katika fainali za Indian Wells mwezi machi mwaka huu