MBWANA SAMATTA ANA SIKU 55 ZA KUJIANDAA KUPAMBANA NA VAN DIJK
UEFA Alhamisi ya Agosti 29 walichezesha droo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2019/2020 na kupanga makundi nane yatakayojumuisha timu nne kila Kundi.
Kwa upande wa Tanzania ilikuwa inasubiria kufahamu KRC Genk ya nchini Ubelgiji inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta watakuwa Kundi gani.
Genk wapo Kundi E na timu za Napoli ya Italia , Salzburg kutoka Austria naLiverpool ya nchini England, timu ambayo safu yake ya ulinzi inaongozwa na beki bora Ulaya na mchezaji bora wa Ulaya Virgil van Dijk ambapo Samatta atakutana na wakati mgumu wa kupamba nae.
Mchezo kati ya Genk na Liverpool utachezwa Oktoba 23 yaani ni siku 55 baadae ambapo Genk atakuwa nyumbani hivyo Samatta ana siku 55 za kujiandaa kabla ya kufikia tarehe ya mchezo huo.
Ratiba kamili ya Genk UEFA Klabu Bingwa Ulaya msimu huu
•Septemba 17 FC Salzburg vs KRC Genk
•Oktoba 2 KRC Genk vs Napoli
•Oktoba 23 KRC Genk vs Liverpool
•Novemba 5 Liverpool vs KRC Genk
•Novemba 27 KRC Genk vs FC Salzburg
•Desemba 10 Napoli vs KRC Genk