LIVERPOOL YAMTIA ‘STRESS’ BINAMU WA STEVEN GERRARD
Mshambuliaji kinda wa Liverpool Bobby Duncan ,18, ameripotiwa kukasirishwa na kitendo cha Liverpool kumzuia kwenda kwa mkopo katika klabu ya Fiorentina ya nchini Italia.
Fiorentina imetuma ofa ya pili ya kutaka kumsajili kwa mkopo mchezaji huyo lakini Liverpool inadaiwa wameipiga chini kitu ambacho kinamkwanza Bobby Duncan.
Wakala wa mchezaji huyo Saif Rubie jana ameandika taarifa rasmi kuelezea kuhusu suala la mteja wake. Wakala huyo amesema kuwa kitendo cha Liverpool kumzuia kijana huyo kuondoka kwenda sehemu ambayo anaitaka kimepelekea kumuathiri kiakili.
Katika taarifa hiyo wakala huyo amesema kuwa kutokana na kukataliwa kwa dili hilo kijana Duncan hajatoka chumbani kwake kwa siku nne mfululizo kwa sababu ya msongo wa mawazo kufuatia kuzuiliwa kuondoka Anfield.
Upande wa wawakilishi wa kinda huyo umethibitisha Duncan hatarejea tena Liverpool na yupo tayari kupigwa faini yoyote.
Duncan ni binamu wa mchezaji wa zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa ni kocha wa Rangers Steven Gerrard ya Scotland.