KEVIN DE BRUYNE KAMKINGIA KIFUA KOMPANY KWA KUVURUNDA
Kiungo wa Manchester City Kevin De Bruyne akifanya mahojiano na Sky Sports ameonekana kumkingia kifua mchezaji mwenzake wa zamani Vincent Kompany ambaye kwa sasa ni kocha mchezaji wa klabu ya Anderlecht kutokana na kutofanya vizuri na timu hiyo.

“(Kompany) amekuwa kocha kwa takribani miezi miwili hivyo unatarajia nini? kwenda pale kushinda kila mechi? hakuna kitu kama hicho katika mpira, ninafikiri kuna idadi kubwa sana ya watu wanaotaka afeli, kwa sababu kufanya kazi hii kuwa kocha mchezaji baadhi ya watu hawapendi lakini namjua Vinny (Kompany) yupo vizuri yamkini hatojali watu wanasema nini” alisema Kevin De Bruyne
Tukukumbushe Kompany ,33, alitangaza kuondoka klabu yake ya zamani ya Man city na kuamua kujiunga na Anderletch kama kocha mchezaji msimu huu lakini amekuwa na mwanzo mbovu katika Ligi Kuu Ubelgiji akiiongoza katika michezo 5 bila ushindi wakipoteza michezo 3 sare 2.