KIPI ATACHAGUA SAMATTA KUCHEZA WORLD CUP NA TAIFA STARS AU UBINGWA WA CHAMPIONS LEAGUE AKIWA NA GENK?
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta akiwa katika klabu yake ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji alifanya mahojiano na Radio GRK na kujibu maswali mbalimbali kuhusu maisha yake ya soka.
Akiwa katika mahojiano na mtangazaji wa Radio GRK Sander Di Monaco alimuuliza kama atakuwa na uamuzi wa kuchagua kipi atachagua, kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Genk au kucheza Kombe la dunia akiwa na Tanzania?
.
“Hilo ni swali gumu kidogo,nitachagua kucheza Kombe la dunia nikiwa na Tanzania hicho ninafikiri ndio kitakuwa kitu muhimu, kwa sababu ni ngumu kuliko Genk kuwa Bingwa au kucheza fainali ya Champions League, nadhani Genk wanaweza kumudu kufanya hivyo kwa miaka ya baadae kutwaa (UCL) lakini kwa Tanzania bado huoni mwanga wa hilo” alisema Samatta