USHINDI MMOJA NDANI YA MIEZI SABA, HUDDERSFIELD YATIMUA KOCHA
Klabu ya Huddersfield ambayo ilishuka daraja msimu uliopita kutoka Ligi Kuu ya nchini England imeamua kumtimua kocha wake Jan Siewart.
Maamuzi hayo yameafikiwa usiku wa Agosti 16 2019 huku wengi wakihoji kuwa mbona wamechelewa kufanya hivyo wakidai kocha huyo alitakiwa afukuzwe kazi siku nyingi kwani haiwezekani kuiongoza timu ndani ya miezi 7 na kushinda mechi moja tu.
Siewert alijiunga na Huddersfield Januari kumrithi David Wagner aliyeondolewa kwa timu kuwa na matokeo mabovu EPL, ndani ya miezi 7 ya Siewert ameshinda mchezo mmoja kati ya 19 akipoteza michezo 15 na sare mechi tatu.
Kipigo cha nyumbani cha 2-1 kutoka kwa Fulham jana usiku,ndiyo kiliweka sahihi katika barua yake ya kufutaa kazi