ALEX IWOBI KAWEKA WAZI OFA YA EVERTON ILIKUWA NGUMU KUIKATAA
Moja kati ya uhamisho uliyokuwa hautarajiwi kuonekana ukitokea katika dirisha la usajili la majira ya joto lililofungwa England ni pamoja na uhamisho wa Alex Iwobi kutoka Arsenal kwenda Everton.
Alex Iwobi aliyecheza michezo 51 ya Arsenal ya mashindano yote msimu ulioisha na kufunga magoli 6 na pasi za usaidizi wa magoli 9 kaweka sababu zilizomfanya aondoke Arsenal timu ambayo imemlea.
“Ofa ilikuwa ya kuvutia sana nisingeweza kuikataa, meneja aliniambia hii ni sehemu ambayo una nafasi na tutakujali na vitu vingine vingi ambavyo mchezaji angependa kusikia, alinifanya nijiamini, nipo tayari kwa changamoto mpya na kuanza ukurasa mpya wa maisha yangu” alisema Iwobi
Mnigeria huyo,23, amejiunga na Everton kwa ada ya Pauni Milioni 35 na kusaini kandarasi ya miaka mitano.