MAN CITY WAPONEA RUNGU LA ADHABU YA USAJILI TOKA FIFA
Uongozi wa Manchester City umefanikiwa kuepuka adhabu ya kufungiwa kufanya usajili licha ya kudaiwa kukiuka sheria ya usajili ya FIFA kwa kumsajili mchezaji wa kigeni aliyekuwa chini ya umri wa miaka 18.
Manchester City wamefanikiwa kuepuka adhabu hiyo baada ya kukiri kutenda kosa la kukiuka sheria hiyo ya FIFA na kueleza kuwa waliitafrisi vibaya sheria hiyo ya usajili, na sasa wamepewa adhabu ya kupigwa faini ya Pauni 315,000 (Tsh Milioni 873)
City walivunja sheria hiyo kabla ya Disemba 2016 ikiwa ni matokeo ya kuitafsiri vibaya.
Sheria za FIFA za usajili wa wachezaji haziruhusu mchezaji aliyechini ya umri wa miaka 18 kusajiliwa na klabu ya iliyo nje ya mipaka ya nchi yake.
Mchezaji wa nchi nyingine atasajiliwa kwa vigezo vitatu.Wazazi wa mchezaji wawe wanahamia kwenye nchi ambayo klabu mpya ipo kwa sababu zisizo za mpira.
Klabu zote mbili ziwe chini ya Umoja wa Ulaya au eneo la kiuchumi la Ulaya na mchezaji awe na umri kati ya miaka 16 na 18. Na pia, klabu inayomununua mchezaji inatakiwa kukidhi vigezo vinavyohusiana na elimu, mazoezi, hali ya maisha na support pamoja na (Wazazi na mchezaji) wawe wanaishi ndani ya Kilomita 100 za klabu hiyo ya ng’ambo.